WATUMISHI WAASWA KUFANYA KAZI KWA WEREDI
Kikao cha watumishi idara ya elimu na watendaji wa Kata kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Msalala na kuhudhuriwa na walimu wakuu , waratibu elimu kata, Maafisa elimu kata, Mgavi, Afisa
mipango , Mhasibu wilaya, Afisa utumishi Wilaya. Ambapo kikao hicho kiliendeshwa na kaimu Mkurugenzi wa
Halmashuri ya Msalala Ndg. Masatu Mnyoro , kikao hicho kilikuwa na lengo la kuwakumbusha watumishi
namna bora ya uwajibikaji katika mazingira yao ya kazi ambapo Kaimu mkurugenzi aliwaambia walimu
wakuu na watendaji hao kuwa na ushirikiano wa karibu na watu wanao waongoza ilikuweza kufanikisha kwa
pamoja shughuli za Serikali kwani mafanikio ya pamoja ni mafanikio ya Halmashauri na si ya mtu binafsi pia
aliwapongeza walimu kwa kufanya vizuri kwenye Mfumo wa FFARS kwani wamekuwa wakifuata utaratibu kama
ambavyo wamekuwa wakielekezwa. Sambamba na hilo Ndg. Mnyoro aliwataka walimu kutambua gharama ya
samani zote wanazo kuwa wanapewa toka Halmshauri.
Afisa manunuzi Ndg. Lorand nae aliwakumbusha wahasibu wa shule na walimu wakuu hao kuwa ni lazima
wanapo fanya manunuzi yoyote ya Serikali ni muhimu kufuata uataratibu wa manunuzi ya Serikali ambayo ni
kama vile kupitisha fomu za ushindani wa bei ambapo aliwahimiza wahasibu kufanya hivyo kutawasaidia
kuwapata wazabuni wenye bei nzuri
Afisa elimu Ndg. Julius Buberwa nae aliwaagiza walimu kuwa na utaratibu wa kuweka wazi mapato na
matumizi ya shule ilikupunguza maswali kwa walimu wao na Jamii inayo wazunguka kwa ujumla . sambamba
na hilo Afisa elimu aliwaagiza walimu wakuu hao kutunza samani wanazopewa .
Afisa Utumishi Ndg. Mary Nziku nae aliwaasa watumishi hao kufanya kazi kwa uweredi na pia kuacha tabia ya
kuwakatisha tama watumishi wanao waongoza kwani wao ndio wapo huko kwa niaba ya Mkurugenzi na
aliwataka pia wakuu hao kuheshimiana na kuthaminiana kwa kufanya hivyo kutawasaidia kuwa na mafanikio
ya pamoja. Ali muomba afisa elimu kuto vyeti vya pongezi kwa walimu wanaofanya vizuri ilikuongeza motisha
kwa watumishi.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.