Watumishi wa Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama wa kada ya utawala ikijumuisha watendaji wa kata 18 na watendaji wa vijiji 92 wamepatiwa mafunzo yenye lengo la kuboresha
utendajikazi wao wa kila siku ili kuweza kuwahudumia wananchi kwa weredi na ufanisi mkubwa na kupunguza kero kwa wananchi.Mafunzo haya yametokana na maelekezo ya waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa ( OR TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa aliyoyatoa kwa Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha watumishi wanapatiwa mafunzo na semina mbalimbali ili
kuwaongezea ujuzi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Mafunzo haya yamefunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji(W) NDG.Khamis Katimba ambaye amewataka watendaji hao kuhakikisha wanatenda haki kwa wananchi wanaowahudumia na kuhakikisha wanawashauri vizuri viongozi
waliopo katika maeneo yao ya kazi na kuwasimamia watumishi waliopo katika kata na vijiji vyao, masuala haya yote yatawezekana iwapo watendaji hao watakuwa mfano kwa watumishi wengine kwa wao wenyewe kufika
ofisini kwa wakati na kutoka saa 9.30 alasiri sambamba na kuwa na lugha yenye staha kwa wateja wanaokuja kupata huduma katika ofisi zao.
Mkurugenzi Mtendaji huyo ameongeza kusema nakutana nanyi mara kwa mara lengo langu kubwa ni kuhakikisha mnaweza kujiendesha wenyewe na kuwaza nini utaifanyia Halmashauri yako na nchi yako kwa ujumla hivyo
tunapokutana kila mtu ana uwezo wa kutoa utaalamu na uzoefu katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku hivyo kuwa rahisi kwa wengine kujifunza kwani mnakutana na changamoto mbalimbali hivyo tunapokutana
tunabadilishana uzoefu na kuimarishana.Natumia gharama kubwa ili kuhakikisha mnasimama na ni matumaini yangu kuwa kero zilizo ndani ya uwezo wenu zinatatuliwa na panaposhindikana tuwasiliane.Simamieni mapato na
kuhakikisha fedha za serikali zinakusanywa ndo maana watendaji wa kata wote nimewapa pikipiki fanyeni ziara za kustukiza ndani ya vijiji ili kuongeza uwajibikaji kwa watumishi wengine nami ntapita kuona hili likitekelezwa
na pale inapoonekana pana uzembe ntachukua hatua,zingatieni tunayoyaelekeza.
Miongoni mwa mada zilizowasilishwa katika kikao kazi hicho ni majukumu ya Mtendaji wa Kata na Kijiji,Vikao vya kisheria vinavyopaswa kufanywa ngazi ya kijiji na kata,chimbuko la Mamlaka za serikali za mitaa na sababu za
kuanzishwa kwake,Dhana nzima ya utawala bora,ukusanyaji mapato na sababu za msingi za kisheria za kwa nini malmaka za Serikali za mitaa zikusanye mapato, masuala ya TASAF na fursa zijazo kwa ajili ya machinga kwani Mhe.Rais
Samia Hassan Suluhu ameelekeza machinga wote kusajiliwa na kutambuliwa hivyo kotoa wito kwa machinga wote kufika ofisi za watendaji wa vijiji kupata maelekezo ya namna ya kujisajili. Mada hizi zimewasilishwa na Mwanasheria wa
Halmashauri wakili msomi Leonard Mabula akishirikiana na mkuu wa idara ya utawala na Usimazi wa rasilimali watu Bi.Mary Nziku ambaye amewataka wana semina kuthamini nafasi walizonazo na kuzitumikia kwa bidii ili kuleta tija ndani
ya halmashauri na kuongeza uwajibikaji na uwazi kwa jamii ambalo ndilo tarajio kubwa la Serikali yetu tukufu ya awamu ya sita.
Kwa upande wao wanasemina,wamepongeza jitihada za Mkurugenzi Mtendaji (W) kwa kuwaamini na kukaa nao mara kwa mara kwani tangu aripoti ndani ya halmashauri semina hii ni tatu ambayo inafanyikia katika jengo la Makao makuu ya Halmashauri
iliyopo katika kata ya Ntobo,pia NDG.katimba amekuwa akitembelea kata na vijiji mbalimbali kila wiki na kukutana na watumishi wa kada za Elimu Msingi na Sekondari,Afya,Kilimo mifugo na umwagiliziaji na kuwakumbusha wajibu wa kazi zao na matarajio
yake kwao."Hongera sana kiongozi wetu nasi hatutakuangusha" kauli hii imetolewa na NDG.Patrick Mahona mtendaji wa kata ya Segese, kwani sasa hivi tunahudhuria vikao vya baraza la madiwani na kuwasilisha taarifa zetu za utekelezaji,suala ambalo linatujengea
uwezo wa kusimama popote.Nae Bi Neema magwega mtendaji wa kijiji cha Ntambalale ameishukuru Halmashauri kwa kutoa mafunzo kwa mabaraza ya ardhi ya kata kwani migogoro mingi iliyopo vijijini ni masuala ya ardhi hivyo sisi kama watendaji wakuu tutayasimamia kwa
ukamilifu na kuhakikisha haki inatendeka.
Mafunzo haya yamehitimishwa na Mkurugenzi Mtendaji(W) NDG.Katimba kwa kuwahakikishia watendaji hao kuwapa Tsh.200,000 kwa kila kijiji na kata kila robo mwaka kwani bajeti hiyo imepagwa,fedha hizi zitumike kununulia vitendea kazi vya ofisi.Pia ntaendelea kuwezesha
mafunzo ya muda mfupi na mrefu nanyi jengeni tabia ya kujiongeza kwa kujisomea mambo mbalimbali ikiwemo miongozo inayotolewa na serikali ili kuongeza upeo wa kujua mambo mengi na kukurahisishia utendaji kazi wako.Simamieni miradi na miundombinu ili kuhakikisha inakamilika kwa ubora
unaotakiwa na mwisho fanyeni mikutano ya kisheria kama inavyotakiwa.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.