Leo tarehe 14/07/2018 ziara ya kikazi ya siku 4 Wilayani Kahama imeanza rasmi ambapo Waziri mkuu MHE. Majaliwa Kassim Majaliwa amepokelewa na umati mkubwa wa wananchi wa Kata ya
Isaka katika Halmashauri ya Msalala, umati huo umeongozwa na Mbunge wa jimbo la Msalala MHE. Ezekiel Maige, Mkuu wa Wilaya ya Kahama ndg. Fadhir Nkurlu, Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Msalala na Viongozi mbalimbali wa chama na Serikali. Wilaya ya Kahama ina Halmashauri 3 ambazo Waziri mkuu atazitembelea na kuzindua miradi mbalimbali za maendeleo
Akimkaribisha Waziri mkuu katika Halmashauri ya Msalala, MHE. Ezekiel maige ametoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya 5 inayoongozwa na Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa jitihada inazozifanya
za kuwaletea maendeleo watanzania ambapo amesema katika jimbo la Msalala kuna miradi mingi mikubwa ikitekelezwa, ameitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni Mradi wa Maji wa ziwa Victoria kutoka
Kagongwa kwenda Isaka ambao utakamilika mwezi Novemba mwaka huu, pana mradi wa kupeleka maji katika kata za Bulyanhulu na Bugarama ambapo mkandarasi yupo eneo la kazi ombi la wananchi wa Msalala
ni kuwa Mkandarasi aongezee spidi ili mradi uanze kutumika. Pia pana upanuzi wa kituo cha Afya Chela sambamba na kupandisha hadhi zahanati za Ngaya na Isaka kuwa Vituo vya Afya ambapo utekelezaji
huu utafanyika katika mwaka huu wa fedha, haya yote yamefanyika kupitia Serikali ya awamu ya tano ikishirikiana na wadau mbalimbali.
MHE. Maige ameendelea kuiomba Serikali kutoa kipaumbele katika ujenzi wa barabara ya Kahama Geita kwani uwepo wa barabara hii utachochea maendeleo kwa watu wa Msalala na kahama kwa ujumla. Mwisho
amemwomba Waziri Mkuu awaeleze wananchi wa Halmashauri ya Msalala hatma ya ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza mabomba kwani pamekuwa na sintofahamu juu ya suala hili.
Katika salamu zake waziri mkuu MHE. Kassim Majaliwa kwa wananchi wa Msalala, MHE. Waziri mkuu amewashukuru wananchi kwa mapokezi mazuri waliyompatia na amewatoa wasiwasi kwa kusema kiwanda cha kutengeneza
mabomba ya kusafirishia mafuta ghafi kitajengwa Isaka kwa kuwa pana miundombinu yote muhimu inayohitajika na hivyo kuwataka wananchi kujenga nyumba nzuri za kulala wageni sambamba na kujenga hoteli nzuri
kwani wageni wengi watakuja kwa kuwa serikali inajenga Reli ya umeme ya Mwanza Dares salaam, Tabora Kigoma Mpanda na Isaka Rwanda ambapo Isaka ni sehemu ya katikati na ni bandari ya nchi kavu hivyo wananchi
wachangamkie fursa hii.
MHe. Waziri mkuu amewataka watumishi wa Serikali kuwatumikia wananchi kikamilifu kwani serikali ya awamu hii haitamvumilia mtumishi yeyote atakaekwenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi.
MHE. Kassim Majaliwa amewataka wananchi wa Halmashauri ya Msalala kuunga mkono jitihada za MHE. Rais za kuwezesha wananchi wanaoishi vijijini kuunganishwa na huduma ya umeme kwani Serikali imeviingiza vijiji
vyote vya Halmashauri ya Msalala katika awamu ya tatu ya utekelezaji wa mradi wa Umeme vijijini ( REA III ). Katika mradi huu MHE. Rais John Pombe magufuli ameshusha gharama za kuunganisha umeme toka Tsh. 380,000
hadi Tsh. 27000 bila kujali nguzo ngapi zitatumika.
Ziara hii itaendelea kesho katika Halmashauri ya Mji wa Kahama na Ushetu na itahitimishwa tarehe 17/07/2018 kwa kutembelea kituo cha Afya Chela na kuweka jiwe la msingi na kuzindua soko na ghala la kuhifadhi mazao
katika kata za Chela na bulige, kata zote zikiwa katika Halmashauri ya Msalala.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.