MAADHIMISHO YA WIKI LA ELIMU KWA MWAKA 2017 MSALALA YATIA FORA
Wiki ya Elimu huadhimishwa kila mwaka kuanzia mwezi wanne mpaka mwanzoni mwa mwezi wa tano. Katika maadhimisho haya Halmashauri ya Wilaya hupata fursa ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa, walimu na shule zilizofanya vizuri. Pia kutoa onyo kwa shule zilizoanya vibaya katika Mitihani ya Kitaifa.
Maadhimisho ya wiki la Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kwa mwaka 2017 yalifanyika katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, ambapo Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama ndugu Timothy Ndanya alikuwa Mgeni rasmi katika warsha hii.
Warsha hii ilipambwa na mazoezi kwa vitendo toka kwa wanafunzi wa shule zinazopatikana katika Halmashauri hii.
Mgeni Rasmi Katibu Tawala (W) ya Kahama ndugu. Timothy Ndanya aliyevaa suti na miwani, Makamu mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Benedicto Manowali aliyevaa suti wa pili kutoka kushoto baada ya Injinia wa Maji ndugu Cyprian ndawavuye akifuatiwa na Mwenyekiti wa kamati ya Elimu, Afya na Maji Mh. Gerald Mwanzia na wajumbe wengine wakiangalia zoezi kwa vitendo la somo la Fizikia.
Mgeni Rasmi Katibu Tawala (W) ya Kahama ndugu. Timothy Ndanya aliyevaa suti na miwani, Mkurugenzi Mtendaji (W) ndugu Simon Berege aliyevaa shati nyeupe na tai, Mwenyekiti wa kamati ya Elimu, Afya na Maji Mh. Gerald Mwanzia mwenye shati la pinki, Mkuu wa idara ya Ardhi na Maliasili, na wajumbe wengine wakiangalia zoezi kwa vitendo la somo la Baiolojia.
Akisoma Risala kwa mgeni Rasmi Afisa Elimu Taaluma kwa shule za msingi ndugu. Euliko Mbaga alisema lengo la maadhimisho ya wiki ya elimu ni Kutoa fursa kwa jamii kuweza kufahamu kwa undani maendeleo ya Elimu ndani ya Halmashauri.
Nae Kaimu Mkurugenzi (W) ndugu Zabron Donge aliongezea kwa kusema Halmashauri ya Msalala imejipanga kuhakikisha huduma nzuri na zenye ushindani zinapatikana kwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kutoa motisha kwa wafanyakazi. Alitoa mfano wa kukamilika kwa ujenzi wa maabara na kuziwekea mifumo ya gesi, ambapo Halmashauri hiyo imekamilisha maabara 13 kati ya 15 na zote zinafanya kazi.
Aliiomba jamii ione umuhimu wa kushirikiana na Serikali katika kufanikisha Elimu bora inapatikana kwani alisema Elimu ndo msingi wa maisha na mwangaza katika mambo mbalimbali hivyo wazazi, walezi na wadau wote tushirikiane kwa pamoja kuleta mabadiliko katika Nyanja ya Elimu Msingi na Sekondari kwa maendeleo ya jamii zetu na taifa kwa ujumla.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.