maelezo haya yamejiri leo tarehe 23/07/2024 katika kikao cha Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango kilichokuwa kikijadili taarifa za utekelezaji za robo ya nne ambapo
kilipokea maelekezo toka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo Wizara ya Afya DR.Saitol Laizer ambaye ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Msalala kwa kuwa na maono ya mbali kwani maendeleo
ya kweli hupatikana mtu anapokuwa na afya bora pasipo kusumbuliwa na maradhi.Halmashauri ya Msalala katika mipango yake ya maendeleo iliamua kujenga chuo cha ukunga na uuguzi
kwa lengo la kuzalisha wataalamu wa sekta ya Afya.
Uamuzi mlioufanya kwa kujenga chuo hiki ni cha kupongezwa sana kwani ni halmashauri chache nchini zenye uwekezaji wa aina hii,halmashauri ya Msalala mpo vizuri sana katika
kuunga mkono kwa vitendo jitihada zinazofanywa na wizara ya Afya nchini hususani idara ya mafunzo hakika ninyi ni wadau wetu hivyo wizara ya Afya idara ya Mafunzo tupo tayari
muda wote kuhakikisha chuo hiki mwaka ujao kinaanza kudahili wanafunzi kwani nimeridhishwa na miundombinu iliyopo sambamba na utekelezaji wa maelekezo tunayoyatoa kila tunapofanya
ukaguzi.Nimemwelekeza Mratibu wa Mafunzo ahakikishe raslimali watu kwa maana ya walimu aanze kuwatafuta ili mei 2025 chuo kianze masomo.
Nae Mratibu wa Mafunzo ameiomba Halmashauri kuhakikisha inakamilisha mabweni mawili ambayo tayari yameshaezekwa kwani mazingira ya chuo kilipo sio rafiki kwa
wanachuo kupanga nje ya chuo kwani bado wanahitaji malezi.Sambamba na hili Halmashauri ijenge nyumba ya mwangalizi wa wanachuo pia iangalie uwezekano ya kupata mtu atakaefuatilia
michakato ya kuanza kwa chuo hiki,ikiwemo mambo ya usajiri wa chuo mapema maana kuna Taasisi lazima zije kukagua ili kuridhia usajiri wake.
Kwa upande wake Myenyekiti wa Halmashauri MHE. Mibako Mabubu amesema mapungufu yote yaliyobainishwa na Wizara ya Afya kupitia Wataalamu wa Idara ya Mafunzo nchini,tumeyapokea na tunaahidi
kuyafanyia kazi mapema ili chuo hiki kianze kupokea wanachuo kwani tunaamini uwepo wa wanachuo kutachochea maendeleo katika maeneo ya Halmashauri yetu sambamba na kutatua changamoto za
upatikanaji wa watumishi wa Afya nchini.Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani kwa mwaka huu 2024/25 tumepanga kuajiri watumishi wa Afya kwa mkataba, yote hii inatokana na sera na mipango
mizuri ya uwekezaji iliyowekwa na Rais wetu DR. Samia Hasain Suluhu.Tunamshukuru pia Mbunge wetu Idd Kassim Idd kwa kutuwakilisha vema kwani bila kufanya kazi kwa umoja mafanikio mnayoyaona yangekuwa ndoto.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.