WORD VISION YAKABIDHI MIRADI ILIYOKUWA IKIISIMAMIA KWA WANANCHI NA SERIKALI.
Sherehe za kukabidhi shughuli zote zilizo kuwa zikifanywa na shirika la Word Vision chini ya usimamizi wa Serikali zimekamilika katika kata ya Busangi ADP ambako ndipo zilipo ofisi za Word vision.Sherehe hizo zilihudhuriwa na wageni mbalimbali ikiwemo Mkuuwa Wilaya ya Kahama ambaye ndiye alikuwa mgeni rasimi,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala,Wakuu wote wa idara pamoja na Wananchi mbalimbali walio jitokeza kutoka vijiji mbalimbali vya kata hizo.
Kabla ya kuanzishwa mradi huo mwaka 2000 kufanyika utafiti wa kina ambapo walibaini changamoto mbalimbali katika sekta zote za Kijamii na Kiuchumi. Nahivyo mradi huu ulianzishwa kwa wakazi wa Kata tatu ambazo ni Ntobo , Busangi na Chela.
Mradi huo umenufaisha zaidi ya Watu 30,553 kutoka kata Tatu ambazo ni Busangi, Ntobo na Chela ambapo wakazi wa kata hizo waliwezeshwa na ADP na kuendelezwa katika shughuli mbalimbali kama vile Ufugaji wa nyuki, Ng’ombe , Mbuzi na Samaki.Shughuli zingine ni kama uhamasishaji na ujengaji wa vyoo, Utoaji wa msaada wa madawati , Ujenzi wa wadi mbili( 2 ) nyumba ya wauguzi Two in one Darubini moja na Solar tatu ( 3 ) katika Kituo cha Afya ch Kata ya Chela.
Mpaka wanafikia kukabidhi miradi hiyo kwa Serikal na Wananchi kwa ajiri ya usimamizi kuendeleza usimamizi shirika hilo limefikisha jumla ya miaka 17. Na hivyo shilika hilo limewakwamu wakazi hao kwa kiasi kikubwa kwani mpaka linafikia kukabidhi miradi hiyo wakazi wake wamejengewa misingi bora ya uendeshaji wa maisha pasipo kutegemea misaada baadhi ya shughuli hizo ni pamoja na Kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao,Chakula na ongezeko la upatikanaji wa vipato ngazi ya familia.
Hivyo wakazi wa kata hizo tatu zilizo guswa na mradi huo zina ushukuru sana mradi wa ADP kwa kuwa mkombozi wa maisha yao.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.