MADIWANI WAFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA MSALALA
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango iliyo kuwa ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala
Mh.Benedict Manuali imefanya ukaguzi wa miradi mabalimbali ndani ya Halmashauri ya Msalala na ikiongozana na
wataalamu mbalimbali toka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo.
Kamati hiyo ilipitia miradi mitatu ambayo ni pamoja na Ujenzi wa barabara toka Mwamboku hadi Nyaligongo na
barabara hiyo Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu walitoa ushauri kuwa barabara hiyo inahitji kuinuliwa kiasi na
kuongezewa madaraja kwani madaraja yaliyopo hayakidhi mahitaji.
Mradi mwingine uliopitiwa na kamati hiyo ni ujenzi wa soko na ghala la kuhifadhia nafaka Kata ya Bulige na
kujionea shughuli mbalimbali za ukamilishaji wa ujenzi huo ambapo unaelekea mwishoni, akizungumza mbele ya kamati
hiyo msimamizi wa Mradi huo Ndg. Maulid Ibrahim kuwa wanatarajia kukamilisha ujenzi huo ndani ya wiki mbili pia
wajumbe wa kamati hiyo waliongeza kuwa kunahitajika kuwekwa bati zinazopitisha mwanga na kuweka mtandao wa
umeme ndani ya jengo hilo.
Sambamba na hilo kamati ya ukaguzi ilipitia mradi wa ujenzi wa bweni la kulala wasichana katika shule ya
sekondari Bulige na kujionea shughuli zilizofanyika pamoja na changamoto zake kwani kalo la choo halijakamilika
kutokana na kalo hilo kujaa maji ya chemichemi pia kamati ilipitia ukarabati wa vyumba vya madarasa vinne
vilivyo fanyiwa ukarabati kwa asilimia miamoja na kupongeza shughuli hiyo.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.