TAARIFA YA YA UKAGUZI WA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA.
Wajumbe baraza la madiwani na wataalamu mbalimbali toka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala wakiongozwa na Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri Hiyo Ndg.Benedict Manuari ilipitia miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri hiyo.
Wajumbe hao walipitia miradi mingi ikiwemo mradi wa nyumba ya mfano Busangi, Ujenzi na upanuzi wa kituo cha afya chela, ujenzi wa chumba cha darasa Chela.
Wajumbe walilizika na namna ya ukamilishaji wa miradi hiyo inavyoendelea kwani baadhi ya miradi hiyo imekwisha fikia hatua nzuri na yakuridhisha, sambamba na hilo Wajumbe hao waliiomba Halmashauri kufanya hima umaliziaji wa jengo la nyumba ya Mwalimu pamoja na darasa moja ililopo kata ya Chela.
Wajumbe waliwashauri wananchi washiriki kulinda na kuitunza miradi hiyo ili idumu kwa muda mrefu ili kuendelea kurahisisha utoaji na upatikanaji wa huduma za kijamii.
Miradi ambayo haijakamilika, kamati walishauri wakandarasi wakamilishe miradi hiyo kwa wakati na pia Serikali ijitahidi kuwalipa wakandarasi kwa wakati.Sambamba na hilo Wajumbe hao waliwataka wananchi wanaofanya kazi za ujenzi wa kituo cha afya Chela wawe wazalendo wa kweli na washiriki kwa pamoja kulinda miradi yote iliyopo katika mazingira yao ili iwe na tija kwao na kwa Taifa.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.