Kauli hii imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji(W) NDG.Khamis Katimba wakati Tafrija
fupi ya kutimisha agizo la MHE. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri
Jeshi Mkuu,lililohitaji jamii kuwezesha wanafunzi katika ngazi mbalimbali kupata
chakula wawapo shuleni ili kuwezesha zoezi la ujifunzaji kufanyika kwa ufasaha.
NDG. Khamis Katimba kabla ya kuanza tafrija hiyo aliomba kuongea na watumishi
wote waliopo kata ya Chela waliohudhuria tafrija hiyo na kuwataka kuwa wazalendo
kwa kutimiza wajibu wao ikiwemo kuwahi mapema kazini na kuhudumia jamii kwani
ndilo jukumu letu kubwa, nae ameahidi kutekeleza haki na maslahi ya watumishi
na kuomba wafanyakazi walioajiriwa hivi karibuni kuwa na subra kwani ndani ya
mwezi huu suala la malipo yao litapatiwa ufumbuzi hivyo amewataka Watendaji
wa kata,Vijiji,Waratibu Elimu kata, walimu wakuu na wafanyakazi wengine kuendelea
kuwasaidia watumishi wapya wakati suala lao likishughulikiwa.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Msalala
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.